jinsi ya kuandaa Tangazo Linalouza.
Natambua umeangaika sana Kuandaa Tangazo (ads) Linalouza kwa haraka.Nataka nikwambie upo sehemu sahihi,endelea kusoma Uzi huu utakusaidia.
Ni vigumu kujua kama utauza au lah Ila Kikubwa ni kujaribu kila aina ya njia.
kuuza kunaanzia kwenye content unavyoiandaa,picha unazoweka,Bei na huduma nyingine.
mitandao mingi ya kuuza na kununua kama Bishoo imekutengenezea Muunganiko wa kukuunganisha na watu wa rika zote kutoka sehem mbali mbali Tanzania.
Ukiandaa Tangazo zuri lenye kuvutia,mtandao wetu utalichagua automatically na kuliweka juu ya mengine.
Ili Mtandao wetu uchague tangazo lako ni lazima tangazo liwe linaeleweka kuanzia Kichwa chake ,picha ,Bei ,usafiri na mahali bidhaa ilipo.Maelezo mengine ya kina usaidia Pia kulipandisha Tangazo lako.
HIVI NI VITU VYA KUZINGATIA UNAPOANDAA TANGAZO.
1: KICHWA CHA TANGAZO (ads title)
Mara nyingi Mtandao wetu unaruhusu maneno yasiyosizidi 50. Unaweza kuandaa kichwa kizuri Chenye kumvutia mteja pale Mara ya kwanza anapoliona tangazo lako.
2:PICHA ZA BIDHAA
Linapokuja Swala la picha hapa ni utulivu yakinifu unaitajika.Huwezi kuuza bidhaa bila kuweka picha yenye kuvutia,wateja wengi upenda kununua picha kwa kuangalia picha tuu.
namna nyepesi ya kuweka picha nzuri ni kupiga picha ya bidhaa zako kwa kutumia simu yako,Weka kitambaa nyuma ya bidhaa ili kuleta background,.piga picha kuanzia pembeni ili bidhaa ionekane vizuri,hakikisha kuna mwanga wa kutosha kusaidia camera .Usitumie picha za wengine au kupakua kutoka mitandaoni.
2
3: Andika maelezo ya kutosha (Product & service description)
Hapa sasa ndo pakujipakulia nyama,kwa maana unalenga kumteka mnunuzi.Andika kadiri unavyoweza Ila maneno yawe mafupi yenye kuleta maana .Elezea bidhaa yako ilivyotengenezwa ,lini ,wapi ,brand na nk.
4: Weka Bei
Hapa sasa ndio mtego ulipo ,unaweza kuandika kichwa kizuri ,picha ukaweka nzuri Ila Bei ukamkimbiza mteja.Fanya utafiti kujua soko lipoje la hiyo bidhaa.weka Bei kwa kuongeza kidgo au kupunguza kidgo kutegemea na utafiti wako kwenye soko.kumbuka wateja uvutiwa na bidhaa zenye bei cheeee!
5:Elezea namna ya kusafirisha bidhaa yako
kama unachaji kusafirisha mzigo basi uweke wazi Ila kuna ukweli unatakiwa kujua wateja wengi upendelea kupelekewa bure (free delivery).kama bidhaa yako ina faida kubwa unaweza kuamua kuwa usafiri bure .