Jinsi ya kuongeza mauzo kwa kutumia duka Mtandao?
Duka Mtandao ni sehemu ambayo unaweza kuweka bidhaa zako kwa mfumo wa picha na bei (digitally)
kama ulivyokuwa kwenye duka la kawaida (local shop) ,duka la mtandao utumia zaidi utepe wako wa kidijitali kunasa wateja.
Watu wengi siku hizi wamekuwa wakisambaza bidhaa zao kwenye Mitandao ya kijamii na pengine hawana duka la kawaida.
kuna pesa nyingi inakupita wewe mfanya biashara ambae hujajua umuhimu wa mtandao.
FAIDA ZA KUTUMIA DUKA MTANDAO.
1: unawafikia wateja wapya
wengi wetu tunategemea wateja wa zamani ambao wanatujua au wanajua tunafanya biashara gani.
kuwafikia wateja wapya umekuwa changamoto na upelekea tuwe na mauzo kiduchu.
2:Ni rahisi mteja kuangalia bidhaa zako zote.
hakuna kitu kinatumia muda kama kutuma picha kila wakati kwa wateja wako .muda mwingine unaweza kuwa busy ukashindwa kuwatumia picha wateja wako .Ukiwa na duka Mtandao ,utaweka bidhaa zako zote sehemu moja na mteja akitaka bidhaa utamtumia link atakutana na bidhaa zako zote zikiwa na bei .
3:Kuongeza Uaminifu na kukuza chapa yako .
unajua hakuna kitu kizuri kama kuwa na biashara ambayo itadumu ata kama utakuwa haupo.
ukiwa na chapa yako nzuri na ukatenngeza jina zuri,wateja watapenda kuwa Karibu yako siku zote na kuiamini bidhaa yako.
unaweza kuwa mkubwa ukianza kuamini kwenye ndoto yako .
4:Inakusaidia kuendelea kuuza ata kama huna bidhaa.
unaweza ukawa huna bidhaa Ila rafiki yako anayo,ukapata mteja kupitia Mtandao na yupo mbali ,unaweza kutoa kwa rafiki yako ukamtumia mteja wako na ukabaki na faida.
5:kuwafikia wateja wa kimataifa.
wateja kutoka nchi jirani wanaitaji bidhaa zako Ila shida hawakujui,fungua duka la mtandao Leo ujulikane.
JINSI YA KUFUNGUA DUKA MTANDAO.
duka Mtandao ni tofauti na akaunti ya mitandao ya kijamii.
bw.kened delly aliwahi kusema
’’instagram isn’t for selling but for sharing’’
mitandao ya kijamii ni kwa ajiri ya kusambaza Ila sio kuuza.
anamaanisha kwamba.
kwenye mitandao ya kijamii wengi utembelea wakiwa na shida zao tofauti ya manunuzi,ingawa wanunuzi wapo.kule unatakiwa kutengeneza machapisho yanayovutia (engaging content) Ili mtu afanye maamuzi ya kununua.
ebu fikiria Wewe upo busy na biashara yako huo muda kuandaa machapisho unatoa wapi?
zipo sehemu za kuuza ambazo watembeleaji wake wanakuja kufuata bidhaa tuu (shopping)
na hizo ni marketplace kama Bishoo .
wateja wanaotembelea Bishoo huja kutafuta bidhaa ili wanunue,wakiona bidhaa kama yako lazima watafanya maamuzi sahihi kununua.
kwahyo sehemu ya kufungua duka la mtandao ni kwenye Mitandao ya kuuza (marketplace)
JE UTAANZIA WAPI KUFUNGUA DUKA LA MTANDAO?